Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) - Mug
Tuna (samaki/jodari) - 2 kopo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 2
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 2 vijiti
Karafuu - 6 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Viazi - 3
Maji - 2 Β½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Maandalizi
Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20 Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu. Tia maji, yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo vya Wali:
Mchele - 3 vikombe
*Maji ya kupikia - 5 vikombe
*Kidonge cha supu - 1
Samli - 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Hiliki - 3 chembe
Bay leaf - 1
Vipimo Vya Kuku
Kidari (chicken breast) - 1Kilo
Kitunguu - 1
Tangawizi mbichi - Β½ kipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili mbichi - 3
Ndimu - 2
Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini - Β½ kijiko cha chai
Jira/Cummin ya unga - 1 kijiko cha chai
Maji - ΒΌ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Wali:
Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto. Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo. Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau. *Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo. *Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.
Kuku:
Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi. Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku. Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri. Tia maji kiasi ΒΌ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)
Updated at: 2024-05-25 10:23:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi
Siagi - ΒΌ Kikombe cha chai
Baking powder - 2 Vijiko vya chai
Pistachio/ lozi - 2 vikombe vya chai
Mafuta - Β½ Kikombe
VIAMBAUPISHI VYA SHIRA
Sukari - 2 Vikombe vya chai
Maji - 2 Β½ Vikombe vya chai
ndimu - Β½ kijiko cha chai
JINSI YA KUANDAA
Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili) Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta. Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na lozi. Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki. Washa moto wa oven 350Β°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana) Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki. Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
ANGALIZO
Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika. Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele Kisamvu kilichotwangwa Samaki Mbaazi Nyanya chungu Vitunguu Nyanya ya kopo Tangawizi Kitunguu swaum Vegetable oil Curry powder Tui la nazi (kopo 2) Chumvi Pilipili Limao
Matayarisho
Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.
Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Mahitaji Ya Nyama
Nyama ya nβgombe ya mifupa - 3Β lb
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Kitunguu thomu - 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau/jira/uzile (cumin) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 cha wastan
Pilipili mbichi - 3 Zilizosagwa
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Muhogo Na Mbatata/Viazi
Muhogo menya na ukate vipande pande - 2
Mbatata/Viazi menya ukate vipande vikubwa kiasi - 5 kiasi
Tui la nazi zito - 1 gilasi
Nyanya ilokatwakatwa au kusagwa - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 kiasi
Bizari ya mchuzi - kiasi
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha nyama kisha weka katika pressure cooker au sufuria. Tia viungo vyote vya nyama uchanganye vizuri, kisha ikorogekoroge mpaka maji yake yakaribie kukauka. Usifunike. Tia maji kiasi ya kuivisha nyama na kubakisha supu yake kiasi ya kuivisha muhogo na mbatata. Muda wa kuivisha nyama inategemea nyama yenyewe na kama unatumia pressure cooker ni takriban dakika 35-40. Ikiwa sufuria ya kawaida utakuwa unaikoroga. Mimina ndani ya supu, muhogo, mbatata, nyanya, kitunguu, bizari ya mchuzi, chumvi. Acha ichemke uive muhogo na viazi. Tia tui la nazi, changanya vizuri acha kwenye moto dakika chache tu. Epua ikiwa tayari. Tolea na achari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga wa ngano vikombe vikubwa 3 Boga lililopondwa kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Sukari kikombe kikubwa 1 Blue band kikombe Β½ Vanilla kijiko kidogo 1 Mayai 2 Maji kiasi/ maziwa (kama nilazima)
Hatua
β’ Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike. β’ Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa. β’ Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa. β’ Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole. β’ Ongeza sukari na changanya. β’ Ongeza mayai na koroga na mwiko. β’ Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike. β’ (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo). β’ Ongeza vanilla na koroga. β’ Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano. β’ Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea. β’ Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive. β’ Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi 6 Nyama ya ng'ombe (nusu kilo) Viazi mviringo 2 Kitunguu swaum Tangawizi Kitunguu maji Nyanya 1 kubwa Mafuta (vegetable oil) Chumvi Limao Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - Β½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - Β½ gilasi
Nazi iliyokunwa - Β½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike. Mimina katika bakuli la kiasi. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350Β° hadi ishikamane na kuwa tayari. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:23:04 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (nusu kilo) Sukari (Kikombe 1 cha chai) Chumvi (nusu kijiko cha chai) Hamira (kijiko kimoja cha chai) Yai (1) Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula) Butter (kijiko 1 cha chakula) Hiliki (kijiko1 cha chai) Maji ya uvuguvugu ya kukandia Mafuta ya kuchomea
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri. Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.