Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia ๐ Sala, ๐ Masomo ya Misa, ๐ Mafundisho, ๐ก Tafakari, ๐ฐ Makala, na ๐ My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
Chezea paka wewe, Angalia kilichomkuta huyu na paka wake
Updated at: 2024-05-25 17:02:32 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa mbal,aliporudi nyumban alimkuta paka amekwisharudi,jamaa alikasirika sana.
Siku ya 2 akamchukua na kwenda naye zaid ya kilometa 50 akapiga chochoro za kutosha kisha akamtupa,akaanza safar ya kurud nyumban baada ya muda akampigia cm mkewe.Vp mke wangu huyo paka yupo? MKE:Ndio mume wangu tena ametulia hapa kwan imekuaje? JAMAA:hebu mpe cm anielekeze njia ya kurud nimepotea๐ณ
Updated at: 2024-05-25 17:07:17 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text "mambo vipi?"โฆhalafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu "shwari"halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Updated at: 2024-05-25 18:09:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee. MALAIKA: Kwa nini? MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni. Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?