Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI YA WALI
Mchele - 3 Magi
Mafuta - 1/4 kikombe
Karoti unakata refu refu - 3
Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa - 1 kikubwa
Pilipli manga - 1/2 kijicho chai
Hiliki - 1/2 kijiko chai
Karafuu ya unga - 1/4 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - 1/2 kijiko cha chai
Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji - 1 kijiko cha chai
Zabibu kavu (ukipenda) - 1/4 kikombe
Chumvi kiasi
KUPIKA WALI
Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo. Tia vitunguu kisha tia bizari zote. Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi Tia mchele upike uwive. Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda. Funika endelea kuupika hadi uwive.
MAHITAJI KWA NYAMA
Nyama - 2 Ratili (LB)
Chumvi - Kiasi
Mafuta - 1/4 kikombe
Kitunguu (kata virefu virefu) - 1 Kikubwa
Pilipili mboga kubwa - 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.
Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.
KUPIKA NYAMA
Chemsha nyama hadi iwive Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu Kaanga kidogo tu kama dakika moja. Tayari kuliwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mashonanguo mkono 1 Tui la nazi kikombe 1 Karanga zilizosagwa kikombe Β½ Mafuta vijiko vikubwa 4 Kitunguu 1 Nyanya ndogo 2 Chumvi kiasi
Hatua
⒠Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata. ⒠Menya osha na katakata kitunguu. ⒠Osha, menya na katakata nyanya. ⒠Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike. ⒠Kuna nazi na chuja tui. ⒠Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike. ⒠Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa, funikiakwa dakika 5 -10. ⒠Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu. ⒠Onja chumvi na pakua kama kitoweo. Uwezekano Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo ki¬dogo au mboga nyingme. Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi. Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya - karanga.
Updated at: 2024-05-25 10:34:39 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ngano nzima (shayiri) - 3 Vikombe
Kuku - Β½ (3 LB takriban)
Thomu na tangawizi iliyosagwa - 1 kijko cha supu
Pilipili manga ya unga - Β½ kijiko cha chai
Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) - Β½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Samli ya moto - Β½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri. Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta Β½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Updated at: 2024-05-25 10:34:51 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni Β½ Magi
Siagi iliyoyayushwa 125Β g
Nazi iliyokunwa Β½ Magi
Mjazo wa karameli (Caramel filling)
Syrup 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa 125Β g
Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)
Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)
Chokoleti 185Β g (dark chocolate)
Mafuta 3 Vijiko vya chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30Β cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.
3. Choma kwenye moto 325ΛC kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.
4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.
5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.
6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Hoho la kiajani 1/2 Njegere 1 kikombe cha chai Carrot 1 kubwa Broccoli kidogo Cauliflower kidogo Kitunguu 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry power 1 kijiko cha chakula Coriander powder 1 kijiko cha chai Tarmaric 1/2 kijiko cha chai Olive oil Chumvi 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Kuku 1 mkate vipande vipande
Vitunguu 3 katakata (chopped)
Nyanya 5 zikatekate (chopped)
Tangawizi mbichi ilokunwa au ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Thomu (kitunguu saumu) kilosagwa kijiko 1 cha kulia
Bizari mchanganyiko (garam masala) kijiko 1 cha chai
Jira/bizari ya pilau (cummin powder) kijiko 1 cha chai
Dania/gilgilani ilosagwa (coriander powder) kijiko 1 cha chai
Mtindi/maziwa lala (yoghurt) vijiko vya kulia 4 mjazo au paketi moja ndogo.
Malai ya kupikia (cooking cream) kikombe 1
Kasuri methi (majani makavu ya uwatu/dried fenugreek leaves) 1 kijiko cha kulia
Mafuta ya kupikia Β½ kikombe
Chumvi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha kuku vizuri mwache achuje maji. Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi ya brown hafifu. Kisha tia tangawizi na thomu ukaange. Tia kuku ukaange mpaka ageuke mweupe kisha tia nyanya endelea kukaanga ziwive. Piga mtindi vizuri katika kibakuli uwe nyororo. Epua sufuria weka kando kisha tia mtindi uchanganye vizuri pamoja na kuku. Rudisha katika moto acha uchanganyike na kuku kidogo kisha mwagia malai ya kupikia (cooking cream) Tia kasuri methi/majani makavu ya uwatu yaliyovurugwa. Acha katika moto dakika 1 tu. Epua umimine katika chombo na nyunyizia ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
1 kilo unga wa ngano 240 ml maji ya vugu vugu 2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula 2 asali kijiko kidogo cha chai 1 chumvi kijiko kidogo cha chai 1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai
JINSI YA KUPIKA
Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10. Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi. Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo. Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara. Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu. Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya. Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa. kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga. Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini. Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 - 450Β F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.
NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.
Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.