Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ngβombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee.
Baadhi ya wapishi wameweza kubuni aina hii ya upishi ambayo huweza kupikwa kwa dakika tano tu na kukupa chakula kitamu chenye ladha ya kuvutia.
Uzuri wa chakula hi ni kwamba kinaweza kuliwa wakati wowote na kwa chakula chochote kulingana na matakwa ya mlaji.
Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya mapishi, biringanya ni miongoni mwa vyakula vyenye mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele. Hapa tutaenda kuona jinsi ya kupika roast ya biringanya na mayai.
Mahitaji:
Biringanya 2 kubwa Nyanya 4 kubwa Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani Mayai 2 Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani Chumvi kiasi Pilipili 1 (kama unatumia) Hoho 1 Karoti 1 Kitunguu swaumu kilichosagwa 1 Kotimili fungu 1
Maadalizi:
Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo. Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia. Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu. Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili. Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri. Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili. Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi 6 Nyama ya ng'ombe (nusu kilo) Viazi mviringo 2 Kitunguu swaum Tangawizi Kitunguu maji Nyanya 1 kubwa Mafuta (vegetable oil) Chumvi Limao Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:35 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 3 vikombe
Samaki Nguru (king fish) - 5 vipande
Vitunguu - 2
Nyanya/tungule - 4
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Pilipili mbichi - 5-7
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7-9 chembe
Kotmiri - 1 msongo (bunch)
Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 2-3
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha samaki, kata vipande kiasi weka kando. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo sana (crush) . Katakata kotmiri weka kando. Saga pamoja, pilipili mbichi, kitunguu thomu, ndimu na chumvi. Changanya pamoja na bizari ya samaki kisha paka katika vipande vya samaki acha kidogo vikolee. Weka mafuta katika sufuria au karai, kaanga vitunguu kidogo tu kisha tia nyanya/tungule endelea kukaanga hadi vilainike na kupondeka. Tia kikombe kimoja na nusu cha tui la nazi, kisha tia vipande vya samaki na masala yake, acha mchuzi uchemke samaki aive. Ongeza chumvi, ndimu, pilipili ikihitajika. Ongezea tui lilobakia acha motoni kwa daika chache tu. Epua mwagia kotmiri mchuzi ukiwa tayari.
Pika wali wa maji/mweupe kama kawaida utolee na mchuzi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mackerel 2 Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2 Limao (lemon) 1/2 Chumvi (salt) kiasi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Coriander powder 1/2 kijiko cha chai Mafuta 1 kijiko cha chai
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Dagaa waliokaushwa (dried anchovy 2 kikombe cha chai) Bamia (okra 5) Nyanya chungu (garden egg 5) Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai) Nyanya (fresh tomato 2) Kitunguu (onion 1) Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai Turmeric powder 1/2 kijiko cha chai Limao (lemon 1/2) Chumvi (salt kiasi) Pilipili (scotch bonnet 1) Mafuta (veg oil)
Matayarisho
Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, turmeric, bamia na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike. Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:54 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)
Sukari 1/3 Kikombe cha chai Mayai 5
Siagi 4 Vijiko vya chakula
Hamira 1 Kijiko cha chakula
Baking Powder 1 Kijiko cha chai
Vanilla 1 Kijiko cha chai
Hiliki zilizosagwa 1 Kijiko cha chai
Sukari ya laini ya unga
(icing sugar) 1 Magi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.
Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.
Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.
Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome. Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nini maana ya lishe?
β’ Lishe yahusu mafunzo ya chakula na jinsi miili yetu inavyotumia chakula kamakichocheo cha ukuaji, kuzaana na utunzaji wa afya. β’ Lishe inajumuisha mchakato wa utoaji virutubishi vinavyohitajika kwa afya, ukuaji, kuendelea na kuishi.
Umuhimu wa lishe bora
Lishe bora ni muhimu katika mambo yafuatayo
β’ Utoaji nishati ili kuishi, uwepo wa mwendo, utendaji kazi, na joto. β’ Ukuaji, uendeleaji, ujengaji mwli, urejeshaji na utengenezaji wa seli na mikusanyika ya seli hizo (tishu) β’ Ufanyaji michakato ya kikemia kama vile uyeyushaji chakula, umetaboli na utunzaji mwili. β’ Kinga dhidi ya magonjwa, upigaji vita maambukizi na uponaji magonjwa. β’ Ili afya njema iweze kudumishwa, mlo wa kila siku lazima ukamilishe shughuli nne zilizotajwa hapo awali. Vyakula vinavyokamilisha moja au zaidi ya shughuli tatu huitwa virutubishi.
Virutubishi
Aina za irutubishi vikuu tunavyohitaji kwa wingi. Hivi ni:
β’ kabohaidreti (vyakula vya wanga, sukari na vyakula vya ufumwele): β’ mafuta yatokanayo na wanyama - haya yapo ya aina kadhaa β’ Protini- kuna mamia ya aina mbalimbali za protini. β’ Maji.
Virutubishi vidogovidogo tunavyohitaji kwa kiwango kidogo. Kuna aina nyingi ya hivi bali vile vinavyoelekea kukosekana kwenye mlo ni:
β’ madini β madini ya chuma (angalia Kisanduku cha 6, ukurasa 16), madini ya joto na zinki. β’ vitamnini β vitamini A, vitamini za kundi B (ikiwemo folate) na vitamini C. Kama chakula chaweza kuwa chanzo bora cha kirutubishi au la hutegemea: β’ Kiwango cha kirutubishi katika chakula. Vyakula vyenye viwango vingi vya virutubishi vidogovidogo kulinganisha na viwango vyake vya nguvu huitwa vyakula βvilivyosheheni virutubishiβ (nutrient-rich) au wakati mwingine huitwa vyakula vyenye βujanzo mwingiβ wa virutubishi (nutrient dense). Vyakula hivi hupendwa kwa kuwa hutoa virutubishi vyote vinavyohitajika. Kiambatisho hiki kinaorodhesha vyakula vinavyotoa viwango muhimu vya virutubishi mbalimbali. β’ Kiwango cha chakula kinachotumika mara kwa mara.