Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 1 Kikombe
Sukari ya kusaga - 3/4 Kikombe
Siagi - 125 gms
Yai - 1
Baking powder - 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu - 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) - 2 Vikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri. Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni. Pika katika moto wa 350ΒΊF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania. Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi.
Aina hii ya mboga kama zilivyo mboga zingine za majani ni nzuri na muhimu kwa afya ya binadamu. Aina hii ya mboga huleta virutubisho mbalimbali mwilini. Hapa tunaenda kuona mapishi ya kisamvu kwa kutumia mafuta bila nazi kama ilivyozoeleka na wengi.
Mahitaji :
β’ Kisamvu kilichotwangwa na kuwa laini β’ Kitunguu maji β’ Kitunguu swaumu β’ Kunde mbichi β’ carrots β’ Mafuta ya kula β’ Chumvi kiasi
Maandalizi :
β’ Chemsha kisamvu ukiwa umechanganya na kunde mpaka uhakikishe vyote vimeiva. Baada ya kuiva weak pembeni. β’ Chukua sufuria kavu, weak mafuta kasha weak katika jiko na yakipata moto weak kitunguu na koroga mpaka kibadilike rangi kasha weak kitunguu swaumu na endelea kukoroga kwa muda baada ya hapo weak carrots na kisha weka kisamvu chako ambacho kimechanganywana kunde. β’ Endelea kukoroga kwa muda na kasha acha kichemke mpaka uhakikishe mboga yako imeiva vizuri. β’ Mboga hii iko tayari kwa kulikwa na inaweza ikaliwa na wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe Sukari ya icing - 1 Kikombe Siagi - 250 gm Yai - 1 Vanilla - 2 Vijiko vya chai Baking powder -1 Kijiko cha chai Jam - ΒΌ kikombe Lozi - ΒΌ kikombe
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa. Pika (bake) katika oven moto wa 375Β° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama
Updated at: 2024-05-25 10:37:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi laini (Matoke 6) Viazi mbatata (potato 3) Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2) Kitunguu swaum (garlic 6 cloves) Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai) Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo) Vitunguu (onion 1) Pilipili (chilli 1 nzima) Chumvi (salt to your taste) Mafuta (vegetable oil) Limao (lemon 1/2) Curry powder (1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakate vipande vitatu. Wakaushe maji kisha wamarinate na kitunguu swaum,tangawizi, chumvi, na limao kwa muda wa masaa 2. baada ya hapo waoke kwenye oven kwa muda wa dakika 30. baada ya hapo andaa ndizi na viazi kwa kuzimenya na kuziosha kisha ziweke pembeni. Kisha katakata vitunguu maji, Tangawizi, vitunguu swaum na nyanya kisha vitie kwenye blenda na usage mpaka mchanganyiko usagike vizuri. Baada ya hapo tia mchanganyiko katika sufuria na ubandike jikoni, acha uchemke mpaka maji yote yakauke. Maji yakisha kauka punguza moto na utie mafuta, curry powder, pilipili na chumvi. Kaangiza mpaka mchanganyiko uive na baada ya hapo tia viazi na maji kiasi na uache viazi vichemke mpaka vikaribie kuiva kisha tia ndizi na samaki na ufunike. Pika mpaka ndizi na viazi viive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari Β½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ΒΎ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari
Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Ugali:
Unga wa mahindi/sembe - 4
Maji - 6 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chota unga kidogo katika kibakuli uchanganye na maji kidogo . Weka maji mengineyo katika sufuria kwenye moto. Changanya na mchanganyiko mdogo ufanya kama uji. Kisha kidogo kidogo unaongeza sembe huku unakoroga na kuusonga ugali hadi uive.
Vipimo Vya Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi
Samaki nguru - 5 vipande
Pilipili mbichi ilosagwa
Kitunguu maji kilosagwa - 1 kimoja
Nyanya ilosagwa - 2
Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ΒΌ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Ndimu - 2 kamua
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumuosha samaki, weka katika sufuria. Tia chumvi, ndimu, pilipili mbichi ilosagwa. Tia vitunguu na nyanya zilosagwa Mkaushe kwa hivyo viungo, akianza kukauka tia tui la nazi. Acha kidogo tu katika moto tui liwive mchuzi ukiwa tayari.
Vipimo Vya Bamia
Bamia - Β½ kilo takriban
Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai
Methi/uwatu/fenugreek seeds ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Dania/corriander ilosagwa - Β½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - 1 kikombe cha kahawa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katakata bamia kwa urefu. Weka mafuta katika karai, kisha tia bizari zote na nyanya kopo, kaanga kidogo. Tia bamia endelea kukaanga, kisha acha katika moto mdogomdogo ufunike. Kila baada ya muda funua karai ukaange bamia hadi ziwive zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo) Siagi (butter vijiko 2 vya chakula) Yai (egg 1) Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji ya uvuguvugu (warm water) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.
Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Nyanya 1Β kg Maji Iita Β½ Chumvi kijiko kidogo 1 Sukari
Hatua
β’ Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike. β’ Chuja juisi. β’ Pima juisi - vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka kwenya sufuria safi . β’ Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke. β’ Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa kunywa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 Β½ gilasi
Sukari Β½ kikombe
Hiliki Β½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.